WAROMBO
WATU WA KILIMANJARO
WASERI au WAROMBO
MAKALA
Waseri au Warombo ni kabila linalopatikana kaskazini mwa mkoa wa Kilimanjaro,lugha yao rasmi ni kiseri. Waseri wanajishugulisha na kilimo, ufugaji,biashara na kazi za ofisini. Pia wanaweza kufanya kazi zingine kama ufundi n.k
Waseri wanapatikana kwa wingi kaskazini zaidi mwa mkoa wa Kilimanjaro hususani kuanzia maeneo ya Kirongo, Tarakea,Rongai na Holili.
Kiseri ni miongoni mwa makundi ya lugha za kibantu yaliyoainishwa na Malcolm Guthrie.
Tofauti ya waseri na wageni ni kubwa sana hasa katika Lugha pamoja na mila na desturi,ikiwemo chakula chao cha asili na matambiko.
Chakula cha asili cha waseri ni Kitheri,umberere,mabande,ngolowo,irombwe,ng'ande na Mtori.
Hata hivyo kwa sasa Mtori unaliwa na watu mbalimbali ambao sio waseri na hupikwa mahotelini kama chakula.
Tofauti nyingine ya wageni na waseri ipo kwenye kinywaji chao cha asili.inafahamika kuwa wageni wana pombe yao inayoitwa mbege.
Lakini waseri wao ni tofauti kabisa,wao wana kinywaji chao ambacho kinaitwa busa.
Utengenezaji wa busa na mbege ni tofauti kabisa kwani busa huandaliwa na vitu vingine.
Pia wageni hawaijui busa ya waseri kuanza utengenezaji mpaka ladha yake. hii inaonesha jinsi ambavyo hakuna uhusiano wowote kati ya wachaga na waseri.
Pia waseri hapo zamani, walikuwa wanakunywa busa kipindi wakifanya matambiko mbalimbali, kwani ni kinywaji mahususi kinachotayarishwa ili kitumike wakati wa tambiko hadi sasa.
Matambiko ya waseri hufanyika wakati wowote katika mwaka,pia hufanyika kwa lengo la kuiamrisha mizimu kutekeleza mambo mbalimbali. tambiko hufanyika katika mti maalumu ulioandaliwa kwaajili ya tambiko miti hii huoteshwa katika kila kaya kwaajili ya kutunza mazigira na chakula cha mifugo.
Waseri wameenea mkoa wote wa kilimanjaro ingawa ni wachache sana kwa idadi yao ila hutambuana kwa kuelewana katika mazungumzo.
Maoni
Chapisha Maoni