WAPARE NA WAGWENO (WACHAGGA WAISHIO MILIMANI)
WAPARE NA WAGWENO(WACHAGGA WAISHIO MILIMANI)
MAKALA
Makala hii inahusisha maoni ya watu wachache, pia simulizi za Mdomo kutoka Kwa wazee wakiseri wa zamani zenye kurithishwa.
Inasemekana kuwa Wapare yani Wachaga waishio katika milima ya upare na Wagweno yani Wachaga waishio katika milima ya ugweno, Waliweza kupanda katika milima yote iliyopo Kilimanjaro na kujenga juu ya milima hiyo. Lakini walishindwa kuishi katika mlima Kilimanjaro kutokana na Baridi kali hali iliyopelekea wengine kupoteza maisha kwenye mlima huo.
Kitu ambacho huenda watu wengi hawajui ni kwamba wapare na Wagweno(yani Wachaga wa Milimani) hawaongopi kuporomoka kutoka huko Milimani kwani maisha yao ya Milimani ni ya karne nyingi, hivyo wanauzoefu wa kutosha wa kuishi Milimani.
Pia hata ikitokea wakaporomoka, haitakuwa kigezo cha kuwafanya kuacha kuishi milimani.
Wazee wetu wanasema wapare waliwahi kuporomoka huko zamani, lakini bado hawaogopi kuishi juu ya milima.
Kilimanjaro imesheheni milima mingi sana ambayo wapare na Wagweno huishi kwa mfano katika Wilaya za Moshi vijijin huishi kwenye vilima. na hata kule Rombo kuna milima ambayo wapare na Wagweno huishi juu ya milima hiyo Mfano Wanapatikana kwenye vilima vya mamsera Rombo nakadhalika huko hujitambulisha kama Wachaga.
Kutoka katika Simulizi za wazee wa Kiseri walioachiwa.
Wapare ni wachagga kabisa hata tabia zao na mwonekano pamoja na lafudhi inafanana kabisa na lafudhi ya kichagga tangu zamani.
Hizi ni simulizi za mdomo zenye kurithishwa vizazi hadi vizazi kutoka wazee wa kiseri walioachiwa.
Wazee wa kiseri wanasimulia kuwa wapare wanapatikana pia Moshi Mjini,moshi vijijini,Siha na Uru,huko wamejenga juu ya vilima na Wengine kwenye tambarare huko hujitambulisha kama Wachaga na pia wanapatikana Rombo katika Maeneo mbalimbali kama vile katika milima ya Mamsera.
Kule rombo wamejenga kwenye vimilima na wachache wamejenga kwenye tambarare, wakiwa Rombo hujitambulisha kama Wachaga,
Wapare ni wachaga waliojidharau kabisa na kujiona watu wa hali duni.
Pia wakiwa huko Same,Mwanga na Ugweno wengi hujitambulisha kama wapare na Wagweno huku wachache wakijiita Wachaga,wamejitenga na wenzao wachagga kwa kujiita Wapare na Wengine kujiita wagweno.
Maoni
Chapisha Maoni