HISTORIA YA WASERI MAKALA Soma zaidi....
USICHO KIJUA KUHUSU WASERI
Waseri ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro,lugha yao rasmi ni kiseri.
MAKALA
Waseri ni kabila linalopatikana kaskazini mwa mkoa wa Kilimanjaro,lugha yao rasmi ni kiseri. Waseri wanajishugulisha na kilimo, ufugaji,biashara na kazi za ofisini. Pia wanaweza kufanya kazi zingine kama ufundi n.k
Waseri wanapatikana kwa wingi katika wilaya ya Rombo kaskazini zaidi mwa mkoa wa Kilimanjaro hususani kuanzia maeneo ya Kirongo, mpaka Tarakea,Rongai na Holili.
Kiseri ni miongoni mwa makundi ya lugha za kibantu yaliyoainishwa na Malcolm Guthrie.
Neno Rombo ambalo ni jina la wilaya limetokana na chakula cha asili cha waseri kiitwacho Romboe.
Pia neno Kilimanjaro ambalo ni jina la Mkoa limetokana na Jina la mlima Kilimanjaro lenye maana ya mlima wa mizimu Kwa lugha ya Kiseri.
Waseri wanapatikana kwa wingi kuanzia maeneo Kirongo na kuchukua eneo lite la mashashiriki na Magharibi kuelekea kaskazini mpaka Tarakea, Rongai na Holili katika wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Katika shughuli za ufugaji Waseri wanafuga wanyama kama vile Ngombe,Mbuzi,Kondoo na Punda.
Hapo zamani Punda walitumika kusafirisha mizigo na watu,ambapo mzigo ulifungwa kwenye mgongo wa Punda na kusafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine,pia tela la kukokotwa na Punda,lilifungwa sambamba na Punda na kubeba watu na mizigo.
Vilevile waseri wanafuga ndege mbalimbali kama vile kuku,Bata,nk.
Katika maswala ya Tamaduni waseri wamejikita katika Matambiko ya mizimu hadi Sasa, wakati wa Matambiko kinywaji aina ya Busa hutumika.
Reference
Bantu languages
Nyabola, Nanjala (2022-10-13). "Citizenship, Language and Digital Rights: the importance of language in the movement to decolonize technology" . foresight . doi : 10.1108/fs-11-2021-0222 . ISSN 1463-6689 . http://dx.doi.org/10.1108/fs-11-2021-0222 .
Martin, Malin D. (1957-07). "CleidocranialTanzania Dysostosis: Two Cases" . The Guthrie Journal 27 (1): 5–13. doi : 10.3138/guthrie.27.1.005 . ISSN 0882-696X . http://dx.doi.org/10.3138/guthrie.27.1.005 .
Buberwa, Adventina (2023-03-23). "Challenges in the use of foreign language names in Tanzania: A Linguistic Imperialism Theory Perspective" . Language Mirror 20 (1): 115–129. doi : 10.4314/kcl.v20i1.8 . ISSN 0856-552X . http://dx.doi.org/10.4314/kcl.v20i1.8 .
Maoni
Chapisha Maoni