Viongozi wa dini za kigeni wanapata wapi nguvu ya kuingilia mamlaka ya nchi, wanatumwa na wakoloni
Hivi Baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) au hata maaskofu wa madhehebu mengine ya kikristo au hata mashekhe wa kiislamu wanahusikaje kwenye mikataba ya Tanzania.
Tunafahamu kuwa kanisa katoliki ni misingi ya Tamaduni za huko Roma Italia.ingefaa zaidi wangehusika na mambo ya huko Italia.
Dini hizi ni za kigeni tutambue hilo.sasa wanatuingiliaje kwenye mambo yetu sisi watanzania.
Huenda askofu au padre au mchungaji au shekhe ni raia wa Tanzania na ana haki kutoa maoni,
Kutumia Baraza au chama cha kidini kutoa tamko ni kumaanisha kuwa umetumwa na watu wa sehemu dini hiyo inapotoka, kwahiyo tunaweza kusema matamko yanayotolewa na Baraza la maaskofu katoliki huenda yametoka huko Roma Italia ndio maana yake,
Sasa Italia inahusikaje na mikataba ya Tanzania.
Kama unatoa maoni toa kama raia wa Tanzania usitumie vyama vya kidini vya kigeni.
Kwa hatua hizi tunaweza kusema hata viongozi wa dini ni vibaraka wa wakoloni, huwa wanatumwa na wakoloni kutoa matamko aibu kwao. tuwe makini na viongozi wa dini.
Viongozi wa dini wanaweza kutumika na wakoloni na kuliangamiza Taifa tuwe makini sana.
Maoni
Chapisha Maoni