ASILI YA MTU WA KWANZA Soma zaidi.......
MTAZAMO JUU YA ASILI YA MTU WA KWANZA
Huu ni mtazamo wangu binafsi sio Mtazamo wa ukoo wangu wala Waseri.
Watu wa kwanza waliibuka kutoka kwenye matope yaliyo gandamana na udongo laini na miamba laini, wakati wa mvua kubwa. Udongo ulioshikamana na ulioambatana na kimbunga kikubwa ukigandamana na miamba laini,uliweza kumuibua mtu kamili.
Mwanaume na Mwanamke kwa wakati mmoja.
Pia viumbe wengine kama wadudu na wanyama waliibuka pia,kupitia miamba hiyo hiyo na matope. hadi leo hii kuna baadhi ya viumbe ambavyo huibuka wakati wa mvua kubwa kwa nguvu za asili.
Ninaposema nguvu za asili simaanishi Mungu.
Mimea ilianza kuchipua yenyewe bila kuoteshwa kwa nguvu za asili(sio Mungu ni Nguvu za asili)
Watu hao walianza kutazamana bila kujuana. Lakini matope na miamba laini viliendelea kuungana na kuibua watu na viumbe mbalimbali. Watu walikuwa hawazaliani kwa kufanya ngono kama ilivyo sasa. Vijiji viliendelea kuzalisha watu kupitia matope ujiuji yasiyo na mchanga na miamba laini pamoja na kimbunga wakati wa mvua kubwa.
Miaka ilizidi kusonga na watu walikuwa wanakula mimea iliyochipua ,mimea ya mwanzo kabisa katika historia ya binadamu kuchipua ilikuwa Mihogo, Kisha Mahindi na Majani, Kisha Ndizi ,Kisha maharagwe, alafu Mpunga . Ngano ilitokana na mchele baada ya mtu wa mwanzo kumeza mbegu ya mpunga, kisha kuinya mbegu ile iliota na kuzaa Ngano kwa nguvu za asili pia.
Matunda ya mwanzo kabisa kuchipua ilikuwa ni Limao na Embe.
Kwenye Limao kukatoka chungwa,ndimu na chenza na kwenye Embe Matunda mengi sana. Mbegu za Limao zilivyo mezwa na wanyama Kisha wanyama hao kuzinya zilizaa matunda mengine ya chungwa, ilivyomezwa ya chungwa na mnyama aliyemeza kunya ilitoka ndimu, Mbegu ya ndimu ilimezwa pia na mnyama alivyoinya itaota chenza.
Pia wanyama wakubwa walimeza mbegu ya Embe na kutoka matunda mengine kwa utaratibu huohuo wa kula mbegu na kuinya, Ali kadhalika nyasi na miti mbalimbali kwa utaratibu huohuo,kwa nguvu za asili.
Pia jitihada za watu kuifanya Dunia kuwa sehemu salama zilileta mabadiliko makubwa ya kiikolojia.
Watu waliendelea kugundua vitu mbalimbali kama vile silaha na zinaa hivyo kupelekea nguvu za asili kupungua na kutegemea akili ya binadamu zaidi.
Mpaka Sasa akili ya binadamu hutumika zaidi katika ugunduzi na Uvumbuzi.
Huku nguvu za asili zikipuuzwa.
Baada ya mtu kugundua zinaa yani ngono,watu walianza kuzaliana kwa zinaa.
Nguvu za asili zipo mpaka sasa baadhi ya nguvu za asili ni,Kunyesha kwa mvua, kunyesha kwa mvua ni matokeo ya nguvu za asili,pia milipuko ya volkano,Kimbunga na matetemeko ya ardhi, maji kupwa na kujaa baharini ni matokeo ya nguvu za asili, pia ardhi na milima ni matokeo ya nguvu za asili.
Nguvu za asili ni matukio yanatokea yenyewe ambayo yanaweza kuwa ya kiikolojia na kijiografia yasiyo husisha jitihada za binadamu.
Sayari ya Dunia,maji na hewa vilitokana na nguvu za asili.
Nguvu za asili sio Mungu.
Translation
A VIEW ON HUMAN NATURE
This is my personal view, not the View of my clan or Seri people.
The first human beings emerged from the mud that was mixed with soft soil and soft rocks, during heavy rains. The compacted soil that was accompanied by a big hurricane and solidified with soft rocks, was able to create a perfect person.
Man and Woman at the same time.
Also, other creatures like insects and animals also emerged through the same rocks and mud.
The plants began to sprout by themselves without being nurtured by the forces of nature (not God, but the forces of nature)
The people started looking at each other without knowing each other. But the mud and soft rocks kept coming together and giving birth to various people and creatures. Humans were birth through sexual intercourse as they are now. Villages continued to produce people through silty mud without sand and soft rocks along with the hurricane.
Years went by and people were eating sprouted plants, the first plants in human history to sprout were cassava, then corn and leaves, then bananas, then beans, and then rice. Wheat originated from rice after the first man swallowed a rice seed, when stool the rice seed swallowed then the seed was germinated produced wheat by natural forces as well.
The first fruits to sprout were Lemons and Mangoes.
On the Lemon came oranges, lemons and limes and on the Mango there were many fruits. Lemon seeds were eaten by animals. Then the animals harvested them and produced other orange fruits. When the orange was eaten by the animal that ate the lemon, a lemon came out. The lemon seed was also eaten by the animal that ate it and it will grow. Also, big animals swallowed the mango seed and from other fruits with the same procedure of eating the seeds and sprouting them. With the power of nature. Also, human efforts to make the Earth a safe place brought great ecological changes.
Humans continued to discover various things such as weapons and sex, thus leading to the decrease of natural forces and relying more on human intelligence.
Until now, the human mind is mostly used in discovery and invention.
While natural forces are neglected.
@Leader
@Kiongozi
Maoni
Chapisha Maoni