SHAKAZULU NDANI YA KILIMANJARO
UGUNDUZI
TOFAUTI YA WACHAGA NA WASHAKA WOTE WANAPATIKANA KILIMANJARO
Je ni VASHAKA Au WACHAGA?
Hebu fuatilia Kwa Makini huwenda na wewe ukaboresha machapisho na maoni yako juu ya wachaga.
Baada ya utafiti wa takribani Miaka mitano, tumebaini kuwa huwenda Kuna Watu walihamishiwa Kilimanjaro kutokea Afrika kusini kwa sababu kutokana na kupeleka dodoso kule Rombo (Useri na Tarakea) tumebaini kuwa kuna watu wanatambuliwa kwa kiswahili kwa jina la WASHAKA kama wapo wengi, akiwa mmoja anaitwa MSHAKA. Kwa Kilugha(Kiseri) wanatambulika kama "VASHAKA" wakiwa wengi lakini akiwa mmoja anaitwa "MSHAKA"Sasa akili yetu ikatupeleka moja kwa moja Afrika kusini na kufananisha na Watawala wa Kabila za wazulu kutoka eneo linaloitwa kwazulu Natali Kule Afrika kusini, Watawala hawa wa Kabila la shaka na Zulu waliitwa SHAKA NA ZULU wakiwakilisha makabila yao, walikuwa ni ndugu, Lakini baadae ugomvi mkubwa ulitokea kati ya Askari waasi katika himaya ya Zulu iliyopelekea Zulu Kuuawa na Askari wake walioasi jeshi. Kitendo hiki kilimuuzunisha sana SHAKA, hivyo akaamuru Askari wake wawatafute wale Askari walioasi jeshi na kumuua ndugu yake.
Kiukweli Askari wa Shaka waliwapata Askari wale waasi wa Zulu wakiwa wamejitangazia ufalme, Vita kubwa ikatokea kati ya shaka na Askari waasi na Shaka akashinda vita, baada ya shaka kushinda vita Aliunganisha himaya yake na ya ndugu yake Zulu hivyo kutambulika kama SHAKAZULU hivyo jina lake pia likabadilika kutoka SHAKA MPAKA "SHAKAZULU" Watawala wote waliofuata baadae wa Kabila la Shaka na Zulu waliitwa "SHAKAZULU" Hadi leo hii.
Hivyo sisi watafiti tumegundua kuwa hakuna Kabila la "WACHAGA" ila kunaweza kukawa na WASHAKA AMBAO ASILI YAO INAWEZA KUWA NI AFRIKA KUSINI. Kwani wenyeji wa wilaya ya Rombo Wanaopatikana USERI NA TARAKEA Wameweza Kueleza kuwatambua Watu Wanaoitwa WASHAKA(VASHAKA) ndani ya KILIMANJARO. ambao pia wapo Rombo kwa uchache.
WATAFITI TUKATOKA ROMBO TUKAENDA MPAKA MOSHI
Tulivyofika Moshi, tukakuta vitu tofauti na vile tulivyoambiwa kule Rombo. wakazi wa Moshi walieleza kuwatambua Wachaka, Badala ya wachaga. na wakaeleza kuwa watu Wanaopatikana Moshi na Hai ndio wanatambuliwa kama Wachaka.
Sasa sisi kama watafiti tumepata ukakasi juu ya Uwepo wa Kabila la Wachaga katika mkoa wa Kilimanjaro. Tunajua jitihada ni nyingi za kukuza utalii lakini tunatakiwa kuwa wakweli Ili sekta hii iweze kukua na kuleta Tija, kuliko kumdanganya mtalii Huku ukweli upo kwa wazawa, tukitaka kuandika historia ni vema tukawauliza wazawa Ili historia zetu ziwe na ukweli Ndani yake. kwani baadhi ya watalii huwauliza wazawa na kuleta mkanganyiko.
Maoni
Chapisha Maoni