WASERI

 

WASERI

Waseri ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro hasa katika wilaya ya Rombo.Lugha yao rasmi ni kiseri. 

Waseri wanajishugulisha na kilimo, ufugaji,biashara na kazi za ofisini pia huweza kufanya kazi zingine kama vile ufundi nk. 

Katika maeneo mengine ndani ya kilimanjaro waseri wanapatikana kwa uchache. 

Mahali wanapoishi waseri panaitwa Useri hata kama ni mikoa mingine, hivyo katika Kilimanjaro Useri inaanzia kirongo na kuchukua eneo lote la Kaskazini, Mashariki na Magharibi mpaka Tarakea,Rongai na Holili. 

Katika maswala ya Tamaduni Waseri wamejikita katika Matambiko ya mizimu ambayo kwa lugha yao huitwa Mtete. Matambiko ya waseri hufanyika muda wowote katika mwaka. 

Chakula cha asili cha waseri ni Kitheri,umberere,mabande,ngolowo,romboe,ng'ande na Mtori.Hata hivyo kwa sasa Mtori unaliwa na watu mbalimbali ambao sio waseri na hupikwa mahotelini kama chakula.

Jina Rombo limetokana na chakula cha Romboe,ambacho ni miongoni mwa vyakula vya asili vya Waseri.

Pia Jina "Kilimanjaro" limetokana na neno la lugha ya Kiseri lenye maana ya "Milima wa mizimu" kwa lugha ya kiswahili.











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Waislamu hupiga kelele msikitini kila baada ya saa kadhaa

HISTORIA YA TANZANIA

TANGANYIKA IKO KWENYE VITA DHIDI YA NCHI TATU(ZANZIBAR, ZAMBIA NA MALAWI)