WASERI
WASERI
Waseri ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro hasa katika wilaya ya Rombo.Lugha yao rasmi ni kiseri.
Kama ni mtu mmoja anaitwa "Mseri''
Waseri wanajishugulisha na kilimo, ufugaji,biashara na kazi za ofisini pia huweza kufanya kazi zingine kama vile ufundi nk.
Katika maeneo mengine ndani ya kilimanjaro waseri wanapatikana kwa uchache.
Mahali wanapoishi waseri panaitwa Useri hata kama ni mikoa mingine, hivyo katika Kilimanjaro Useri inaanzia kirongo na kuchukua eneo lote la Kaskazini, Mashariki na Magharibi mpaka Tarakea,Rongai na Holili.
Katika maswala ya Tamaduni Waseri wamejikita katika Matambiko ya mizimu ambayo kwa lugha yao huitwa Mtete. Matambiko ya waseri hufanyika muda wowote katika mwaka.
Chakula cha asili cha waseri ni Kitheri,umberere,mabande,ngolowo,romboe,ng'ande na Mtori.Hata hivyo kwa sasa Mtori unaliwa na watu mbalimbali ambao sio waseri na hupikwa mahotelini kama chakula.
Jina Rombo limetokana na chakula cha Romboe,ambacho ni miongoni mwa vyakula vya asili vya Waseri.
Pia Jina "Kilimanjaro" limetokana na neno la lugha ya Kiseri lenye maana ya "Milima wa mizimu" kwa lugha ya kiswahili.
Wakati wa ukoloni Mjerumani alichukua Maneno machache ya lugha ya kiseri na kuyatumia kuunda Kamusi ambayo ilitumika kuwafundisha mitume wa kueneza dini. Kamusi ilitumika kuandika Vitabu vya sala ya pamoja vya madhebu ya Katoliki na Lutheran ambavyo mpaka leo vipo na vinatumika.
Wageni waliletwa na wakoloni kuja kueneza dini mbalimbali zikiwemo ukristo,na Uislamu.
Maoni
Chapisha Maoni