HAIWEZEKANI KUWA NA DINI YA DUNIA

DUNIA HAIWEZI KUWA NA DINI MOJA AU UTAMADUNI MMOJA.

Watu na binadamu tunatofautiana sana, kimawazo, Mila na Desturi na utamaduni. hata katika nchi unaweza kukuta raia wa mikoa na makabila mbalimbali wana Mila na Desturi zao. ambazo ni tofauti sana na watu wa mikoa mingine.

Mfano nchi yetu ya Tanzania Ina makabila zaidi ya 120 wote Hawa wana Mila zao tofautitofauti hawawezi kuungana na kuwa na Mila Moja au utamaduni mmoja. ni ngumu kuwaunganisha Kuna watu wameshajaribu kuwaunganisha ikashindikana.

Watu wanataka Kila Kabila liwe na desturi na utamaduni wake. kinachotakiwa kufanyika ni kuondoa zile Mila kandamizi lakini sio kuwaunganisha ili watambike Kwa pamoja. ni jambo lisilowezekana.

Sasa imeshindikana Ndani ya nchi hivyo hata kidunia haiwezi kuwezekana watu kuwa na Imani Moja. hata tukilazimisha ni kujidanganya sisi wenyewe. na tukiendelea kulazimishwa ni kusababisha migogoro na machafuko hakuna jipya.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Waislamu hupiga kelele msikitini kila baada ya saa kadhaa

HISTORIA YA TANZANIA

TANGANYIKA IKO KWENYE VITA DHIDI YA NCHI TATU(ZANZIBAR, ZAMBIA NA MALAWI)