WACHINA WANAUZA BIDHAA ZAO HAPA KARIAKOO, Hizo Nguo wanazouza,wameshona wao wenyewe

 WACHINA WANAUZA BIDHAA ZAO.


Wachina wanauza bidhaa zao, Kuna vijana wavivu wamekuwa na mijadala mtandaoni hasa wengi wanalalamika wachina kuuza Nguo kariakoo, Huku wao wakishindwa kutambua kuwa Nguo hizo zimetengenezwa na wachina hivyo ni haki yao kuuza Nguo hizo. 


Pia vijana hao wameshindwa kujua kuwa Kariakoo ni soko la kimataifa, ukiondoa wachina wapo pia watu wa mataifa mbalimbali ambao wengine wanauza bidhaa za wachina, kwahiyo wachina ameamua kuja kuthibiti bidhaa zao mwenyewe kwa faida ya nchi yao.


Hebu jaribu kufikiria, bidhaa unatengeza wewe alafu inauzwa na mtu mwingine alafu Anapata faida kubwa kuliko wewe, Lingine, ni kwamba wachina wameshindwa kuajiri watu hasa Wenyeji,kwasababu asilimia kubwa huiba na kusababisha hasara hivyo wameamua kuuza wenyewe, kuepuka wizi nk.


Watu wengi wamekuwa wakiiba fedha na kuzifanyia anasa mbalimbali na kusababisha hasara kwenye makampuni ya wageni,hebu fikiria ingekuwa ni wewe ni hatua gani ungewachukulia hao wanaoiba? 


Dar es salaam ni soko la kimataifa,watu hutoka nchi mbalimbali kuja kununua na kuuza bidhaa Dar es salaam, kwahiyo sio wachina pekee wanajifanya Biashara Kariakoo.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Waislamu hupiga kelele msikitini kila baada ya saa kadhaa

HISTORIA YA TANZANIA

TANGANYIKA IKO KWENYE VITA DHIDI YA NCHI TATU(ZANZIBAR, ZAMBIA NA MALAWI)