MAGUFULI ALIKOPA NA KUFANYA MIRADI YA MAENDELEO KWA MIAKA MINNE PEKEE, SAMIA AMEKOPA FEDHA AZIJULIKANI ZILIPO KWENDA.
SERIKALI YA AWAMU YA TANO CHINI YA DKT JOHN POMBE MAGUFULI WALIWEZA KUTUMIA FEDHA VIZURI NA KUFANYA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO NDANI YA MIAKA MINNE PEKEE.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli iliacha Deni la Taifa likiwa Trillion 61.
MAMBO YA MAENDELEO ALIYOFANYA MAGUFULI BAADA YA KUKOPA KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA UONGOZI WAKE (2015-2019)
1.Ujezi wa Flyover, Madaraja ya juu ambayo yamepunguza ajali Kwa kiasi kikubwa kwenye makutano ya barabara katika jiji la Dar es salaam. Ili kamilika Kwa asilimia mia moja.
2.Ukarabati wa shule kongwe na ujenzi wa Shule Mpya za Msingi na Sekondari, suala lilifanyika Kwa asilimia kubwa sana hadi vijijini. alikamilisha Kwa asilimia mia moja.
3.Ujenzi wa stendi Mpya za kisasa mijini na vijijini, Stendi inayoonekana ni Ile ya mbezi Mwisho kama mfano, lakini zilijengwa nyingine nyingi vijijini. alikamilisha Kwa asilimia mia moja.
4.Kukarabati majengo ya Serikali, ikiwemo halmashauri Kwa kiwango cha juu.
5. Ununuzi wa madawati katika shule za Msingi na Sekondari Kwa kipindi cha miaka Minne pekee, Kila mwanafunzi alikaa Kwenye Dawati.
6.Ununuzi wa ndege Mpya iliyofufua shirika la Ndege. alikamilisha Kwa asilimia mia moja.
7. Ununuzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo vitabu vya kujifunzia, vitabu vilikuwa Vingi sana Mashuleni.
8.Ujenzi wa viwanja vipya vya Ndege.
9. Ujenzi wa bwawa la kufua umeme mwalimu Nyerere, ambalo lilikamilika mwaka 2022, pesa nyingi zilitumika wakati wa Magufuli.
10. Ujenzi wa Ikulu ya Dodoma. alikamilisha Kwa asilimia mia moja.
11. Ujenzi wa Reli ya kisasa ya umeme, Standard gauge railway, Kipande cha Dar es salaam hadi Dodoma, alikamilisha Kwa asilimia mia moja.
DENI LA TAFA AWAMU YA SITA, NI SHILINGI TRILIONI 98, ONGEZEKO NI SHILINGI TRILIONI 37, LAKINI HAKUNA KUTU CHA MAANA KILICHOFANYIKA, JE SAMIA SULUHU HASANI ANASTAHILI KUENDELEA KUONGOZA NCHI?
Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassani, deni la Taifa limefika Shilingi trilioni 98, kutoka Shilingi Trilioni 61,Ongezeko ni Shilingi Trilioni 37, lakini hakuna kitu cha maana kilichofanyika.
Sasa jiulize Samia amepeleka wapi Fedha nyingi kiasi hicho, Kiasi cha Shilingi trilioni 37. za mkopo, Zilizopelekea Deni la Taifa Kufika 98.
MAMBO YA KUJIULIZA KABLA YA KUPIGA KURA KUMCHAGUA SAMIA SULUHU HASANI.
1.Tukimwongezea Samia miaka mingine Mitano deni la Taifa litafika Trilioni ngapi?
2. Je katika miaka Mitano ijayo Samia Suluhu Hassani, alifanyia nini Taifa, kitu kitakachoonekana baada ya kuongezeka Kwa deni la Taifa?
3. Je hizo Trilioni 30, alizokopa kwaajili ya Miradi ya Maendeleo Zimekwenda wapi?
4. Je ametufanyia Nini wananchi Ili tuweze kuamini kuwa, SAMIA SULUHU HASANI, sio mwizi na mbadhirifu wa mali ya umma?
Maoni
Chapisha Maoni